Tuesday, February 8, 2011

KUTOKA BUNGENI na Mwerevu


Waziri Mkuu MIZENGO PINDA leo amewasilisha bungeni kauli yake kuhusu kuanzishwa kwa mchakato kuhusu maoni juu ya marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania.

Kuwasilishwa kwa hoja hiyo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais JAKAYA KIKWETE ambayo aliitoa katika hotuba yake ya mwaka mpya.

Waziri Mkuu PINDA amewataka wananchi wawe huru kutoa maoni yao kuhusu mfumo wa katiba wanaoutaka kabla ya mabadiliko ya katiba hiyo hayajafanyika ili kuendana na matakwa ya vizazi vilivyopo.

Ameeleza kuwa marekebisho hayo ya katiba yanatakiwa kukidhi matakwa ya kizazi kilichopo kwa miongo mitano ijayo.

No comments: