Thursday, February 3, 2011

Wanafunzi wa Sheria Tudarco waandamana hadi ofisini kwa askofu Malasusa

Dakta Masumbuko Lamwai, mkuu wa kitivo cha sheria-Tudarco


Wanafunzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar es Salaam wameandamana leo hadi katika Makao Makuu ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani(KKKT) DMP, kulalamikia mambo kadhaa ambayo wanadai hawaridhishwi nayo chuoni kwao.
Rais Kikwete na Askofu Dakta Malasusa, ktk moja ya picha za pamoja.

Taarifa za kuwepo maandamano hayo zilikuwepo muda tangu asubuhi lakini hata hivyo hawakufanikiwa kufika katika makao makuu ya ofisi za Dayosisi hiyo hadi ilipotimia saa kumi na nusu jioni, ambapo walifika wakiwa na mabango yenye maneno mbalimbali linalosema, "Tunataka ada ipunguzwe", "kanisa lisinyonye wanyonge", na mengineyo.

Hata hivyo, mara baada ya kuwasili mlangoni, wamekutana na ulinzi mkali wa FFU pamoja na mashushu wengine, ambapo baada ya kuimba mlangoni hapo kwa muda alitokea mkuu wao wa kitivo cha sheria cha chuo hicho, Dakta Masumbuko Lamwai, ambaye aliwatuliza na kuwataka wachague wawakilishi watano, ambao wamekwenda ofisini kwa askofu kwa ajili ya kuwasilisha malalamiko yao.

hadi nakwenda mitamboni, bado haijajulikana kama madai yao yatatatuliwa au la.

No comments: