Tuesday, September 13, 2011

HITMA YASOMWA, LEO MWISHO MAOMBOLEZO KITAIFA.


  Wazamiaji wa Afrika Kusini waanza kazi

Watu waliokufa katika ajali ya meli ya Spice Islanders Ijumaa usiku katika eneo la Nungwi, Zanzibar jana walisomewa hitima ya kitaifa iliyohudhuriwa na viongozi wa juu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ). 
Waliohudhuria ni Rais Jakaya Kikwete; Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Mohamed Gharib Bilal; Waziri Mkuu, Mizengo Pinda; Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad; Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd; Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho; Rais Mstaafu wa Muungano, Ali Hassan mwinyi; Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim; mawaziri wa Muungano, SMZ na viongozi wa madhehebu ya dini.

Rais Kikwete akizungumza baada ya kukamilika hitima hiyo, alisema ushirikiano wa vyombo vya ulinzi na usalama vya Muungano na Zanzibar, umesaidia kuokoa watu wengi katika ajali ya meli.

Hata hivyo, alisema mazingira ya giza yaliwafanya waokoaji kuwa katika wakati mgumu, alisema ingawa askari polisi wa Kikosi cha Wanamaji na meli ya jeshi aina Kasa, ilianza safari mara baada ya kutokea ajali.
Chanzo: Ippmedia taarifa kamili;
http://www.ippmedia.com/


No comments: