Thursday, September 8, 2011

MIKOA MIPYA TZ KUTAJWA RASMI KESHO


Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesema Serikali itatoa tangazo rasmi la Serikali kuhusu uanzishaji wa mikoa mipya na wilaya mpya ambalo linatarajiwa kuchapishwa kesho.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Rukwa na wa wilaya ya Mpanda mara baada ya kuwasili katika kiwanja kidogo cha ndege cha Sitalike katika Hifadhi ya Wanyama ya Katavi na kupokea taarifa ya Mkoa na Wilaya.

Amesema wananchi wanapaswa kuzingatia kwamba taarifa zao ni lazima ziwasilishwe makao makuu ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika muda wa siku 30 kuanzia siku ambayo Rais Kikwete alisaini tamko hilo.

Waziri Mkuu amesema hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa zoezi la kuweka mipaka mipya kutoka kwenye wilaya na mikoa ya zamani na kisha kuchora ramani za kuonesha mikoa mipya na wilaya mpya.

Waziri Mkuu PINDA amewasili wilayani humo kwa ajili ya ziara rasmi ambapo anatarajiwa kuzindua matawi mawili ya Chuo Kikuu Huria na tawi la Benki ya CRDB.

Kesho anatarajiwa kuzindua tawi la Chuo Kikuu Huria la Sumbawanga huko mjini Sumbawanga.

No comments: