Friday, September 2, 2011

PINDA KUFUNGUA MATAWI YA VYUO VIKUU


NA SCOLASTICA broken heart KOMBA, DAR

WAZIRI mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhehimiwa MIZENGO PINDA anatarajiwa kuwa mgeni rasimi wa uzinduzi wa ofisi za chuo kikuu huria cha Tanzania -OUT -mikoa ya Rukwa na mkoa tarajiwa wa Katavi ambapo ni chuo kikuu pekee kuanzishwa na kutoa huduma za ngazi ya chuo kikuu katika mikoa hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake katika makao makuu ya muda ya chuo kikuu huria cha Tanzania kilichopo Kinondoni jijini Dar Es Salaam Prof. TOLL MBWETE.

Amesema uzinduzi unatarajiwa kufanyika tarehe 9 mwezi huu kwa majengo ya kituo cha chuo kikuu huria mkoa wa Rukwa wilayani Sumbawanga na tarehe 10 mwezi pia Mheshimiwa PINDA atazindua kituo cha mkoa tarajiwa wa Katavi.
Prof. MBWETE amesema majengo ya ofisi za chuo katika mikoa hiyo yamekarabatiwa kwa fedha za ndani za chuo hicho na kuwa na uhakika wa jengo la mahabara, maktaba na jengo la kuwekea mitihani na kusema kuwa chuo kimejidhatiti rasimi kwa kutoa huduma kwa wanafunzi.

Ameongeza kuwa kuhusu mwa mpya wa masomo wa mwaka 2011/2012 wanafunzi wameshafanyiwa udahili tayari kwa kuanza masomo na kusema katika mkoa tarajiwa wa Katavi kunaongezeko kubwa la wanafunzi wa kozi fupi za kompyuta.
Akizungumzia hatua zilizofikiwa katika kutimiza ombi la wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ofisi za chuo katika maeneo ya bunge ili waweze kuhudumiwa kimasomo hata wawapo katika shughuli zao za kitaifa bunge mjini Dodoma Prof. MBWETE amesema tayari taratibu zimefanyika ambapo hadi kufikia kikao cha bunge cha mwezi wa kumi inatarajiwa kuanza kuhudumia wanafunzi

No comments: