Thursday, October 6, 2011

UBINAFSI-NIUUNAVYO!!

Ubinafsi tu. Kama ni njaa, si wote inauma? Hivi kwa nini ule peke yako, ina maana huoni matumbo ya wenzako?

Ndugu zangu,

Ubinafsi duniani ulianza tangu zamani. Lakini kwa kadri binadamu anavyopiga hatua kimaendeleo, ubinafsi unazidi kukua. Hata hivyo, hakuna jitihada zozote za kijamii angalau za kuhamasisha na kuongeza uelewa wa wanajamii kuhusu madhara ya mtu kuwa mbinafsi.

Kwa tafsiri yangu, Uvunjifu wa maadili, Vita, Ufisadi na mengine mengi ni matokeo ya huu huu ubinafsi kutamalaki.

Pengo kati ya walionacho na wasionacho linazidi kuongezeka. Wengine wanadai hayo ni matokeo ya mfumo wa ubepari ambao unafuatwa na nchi zetu, baada ya ujamaa kuzikwa bila matanga. Hata hivyo, hata huo ubepari tafsiri yangu ni hiyo hiyo ubinafsi. Ila kuna ubinafsi unaopakwa mafuta.

Nawasilisha.

No comments: