Friday, August 26, 2011

BALAA KWENYE JUMBA LA KAMARI MEXICO



Shambulio lililofanywa dhidi ya jengo la kuchezea kamari huko Monterrey, kaskazini ya Mexico, limewauwa watu wasiopungua 53.

Mwendesha mashtaka wa serikali alisema idadi ya watu waliokufa inaweza ikaongezeka, kwa vile shughuli za uokozi bado zinaendelea. Rais Felipe Calderon alililaani shambulio hilo, akiliita kuwa ni kitendo cha ugaidi kinachochukiza na cha kinyama.

Majengo ya kuchezea kamari huko Monterrey hivi karibuni yamekuwa yanalengwa kwa mashambulio kwa vile baadhi ya wamiliki wa klabu hizo wamekataa kulipa fedha za ulinzi zinazotakiwa na magengi ya wahalifu.

Zaidi ya watu 41,000 wamekufa katika michafuko inayofungamanishwa na magengi ya uhalifu wa kupangwa huko Mexico tangu Rais Calderon alipoanzisha msako wa kijeshi dhidi ya magengi hayo hapo Disemba mwaka 2008.

No comments: