Tuesday, August 30, 2011

Kikwete mgeni rasmi Idd DOM

Waislamu mkoani Dodoma wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya Swala ya Idd inayotazamiwa kufanyika Kitaifa mjini humo.

Sheikh wa mkoa wa Dodoma, MUSTAFA RAJAB SHAABAN ametoa wito huo wakati Waislam Duniani kote wanatazamia kuswali Swala ya Idd ikiwa ni ishara ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kutegemea kuandama kwa mwezi mosi maarufu kama SHAWWAAL.

Wakati Waislam Duniani kote wakijiandaa kwa Swala ya Idd, baada ya mwezi wa toba kumalizika kwa kutegemea mwandamo wa mwezi, Sheikh wa mkoa wa Dodoma, MUSTAFA RAJAB SHAABAN anaeleza furaha kwa niaba ya Waislam wa mkoa wake kwa Baraza Kuu la Waislam nchini, BAKWATA kupanga shughuli hii muhimu kufanyika Dodoma.

Swala hiyo ya Idd itafanyika mjini humu ambapo mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, JAKAYA MRISHO KIKWETE, Inshaallah.

No comments: