Wednesday, February 9, 2011

CHADEMA WALIKUWA SAHIHI?




Leo, katika kipindi cha Mada na Hali Halisi kinachorushwa na Radio Upendo, Mada iliyozungumziwa ni kuhusu walichokifanya Chadema jana, kuondoka ndani ya ukumbi wa Bunge kukwepa kuhusishwa kupiga kura kuamua kuhusu hoja ya kambi rasmi ya upinzani bungeni.

kati ya wachangia mada waliojitokeza kuchangia kwa njia ya simu, sms na moja kwa moja, wengi wamewafagilia Chadema kwa maelezo kuwa CCM ina ajenda ya siri katika kuhamasisha vyama vya upinzani viwe na kambi moja ya upinzani, licha ya tofauti kubwa ya kiitikadi na kimaslahi inayoibuka kati ya Chadema, CUF na TLP, ukiachilia mbali NCCR Mageuzi na UDP.

Msimamo wangu uko pale pale, wasanii wasilete usanii katika Bunge ambalo linatakiwa kutuwakilisha. Msimamo thabiti pekee, kama wa jana ndio utatufanya tutoke hapa tulipo.

No comments: