Tuesday, September 13, 2011

VITUKO IGUNGA:MGOMBEA WA CUF AIPIGIA DEBE CCM

Mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga mkoani Tabora kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Leopord Mahona, amesema watu wanaobeza maendeleo yaliyofanywa na Chama cha Mapinduzi (CCM) katika miaka 50 ya Uhuru sio waungwana. 
 “Huwezi kuwabeza CCM (Chama cha Mapinduzi), utakuwa ni mtu wa ajabu kama ukianza tu kuongea hawajafanya kitu, sidhani kama ni ungwana CCM have done something (wamefanya kitu). Mimi naamini wamefanya kitu, ila ni wamefanya kwa kiwango gani,” alihoji na kuongeza:“Wamefanya kwa kiwango wanachoweza, uone kiwango walichokomea, huwezi kuzungumza kwamba hakuna maendeleo kabisa, yapo unaweza ukaona na unaweza ukaambiwa na unaweza hata ukashika.”

Mahona alibainisha iwapo atachaguliwa atashirikiana na wananchi kuanzisha vyama vya Ushirika wa Kuweka na Kukopa (Saccos) katika  kila tarafa zote za jimbo hilo huku akichangia Sh. milioni nne kwa vyama vinne vitakavyoanzishwa.

Pia alisema asilimia 15 ya mshahara wake wa ubunge atauingiza katika Saccos zitakazoendeshwa na wananchi wa tarafa husika.

Meneja wa kampeni wa mgombea huyo, Antony Kayanga, alibeza hatua ya CCM kutangaza kuwa Igunga ina maji mengi ambayo yaliwezeshwa na mbunge aliyejiuzulu, Rostam Aziz.

“Wamekuwa wakitangaza Igunga ina maji mengi sambayo Rostam Azizi amechimba mabwawa. Hili nasema Rostam Aziz hajachimba mabwawa isipokuwa amechimba vishimo,” alisema.
CHANZO: NIPASHE

No comments: