Wednesday, February 16, 2011

Siku moja baada ya Valentine, Leo Maulid,


mtume Mohamad alivyotengeneza Kaaba huko Maka

Maulid (pia: maulidi), Maulid an-Nabii ni sikukuu ya dini ya Uislamu ya kuzaliwa kwake Mtume Muhammad.

Neneo lenyewe ni la asili ya kiarabu kutokana na مولد النبي (maulid an-nabi) au (milaad an-nabi) ميلاد النبي . Sikukuu inafuata kalenda ya Kiislamu. Waislamu wa dhehebu la Sunni husheherekea tar. 12 Rabi'-ul-Awwal na Waislamu wa dhehebu la Shia husheherekea tarehe 17. Rabi'-ul-Awwal. Muhammad alizaliwa takriban mwaka 570 BK.

Wataalamu wa historia wengine wanasema ya kwamba sherehe ya Maulid imeanzishwa mnamo karne ya 12 BK. Kuna Waislamu kadhaa wanaokataa sherehe hiyo kwa sababu hakuna sunna wala hadith ya Muhammad mwenyewe kuhusu kusheherekea maulid yake. Lakini kwa ujumla ni sikukuu inayopendwa sana na Waislamu wengi duniani.

Kati ya desturi ni mikutano, kusikia mashairi juu ya maisha ya mtume a mengine. Misri maulid ni kati ya sikukuu za kiislamu zinazokumbukwa sana na Waislamu. Katika Afrika ya Mashariki sherehe ya maulid huko Lamu imejulikana hasa ikivuta wageni kutoka pande zote za Afrika ya Mashariki hadi Uarabuni.

Maulid njema....!

No comments: