Wednesday, August 24, 2011

BUNGE KUUNDA KAMATI TEULE KUCHUNGUZA SAKATA LA DAVID JAIRO


Mheshimiwa Zitto Kabwe leo amewasisimua wabunge baada ya kutaka bunge lizuie shughuli zote za serikali ili kujadili sakata la david Jairo.

Kwa mujibu wa hoja ya Zitto, Kitendo cha Katibu Mkuu Kiongozi kumsafisha David Jairo ni dharau kwa bunge na pia kwa Waziri Mkuu ambaye alishasema bungeni kwamba katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Nishati na Madini atawajibishwa kinidhamu na mamlaka iliyomteua.



Sisi yetu macho, tunaangalia hili sakata litaishia wapi, ila ingekuwa nchi nyingine, asingelala mtu mpaka kieleweke.

No comments: