Friday, February 4, 2011

Uchakachuaji wa mafuta watafutiwa dawa

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA),imepata mashine nne za kupima vinasaba kwenye mafuta ili kudhibiti vitendo vya uchakachuaji vinavyofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wa mafuta wasio waaminifu.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa EWURA, Bwana TITUS KAGUO amesema kuwa mashine hizo zinazojulikana kwa jina la XRF zitafungwa kwenye magari ambayo yatakuwa yakizunguka nchi nzima ili kufanya ukaguzi huo.

Amesema mradi mzima wa kufanya ukaguzi huo umegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni mbili ili kuondoa tatizo la uchakachuaji wa mafuta hayo.
Bwana KAGUO ameeleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara ambao si waaminifu wanaochaganya mafuta hayo watagunduliwa mara moja na hatua za kisheria zitachululiwa dhidi yao.

Amebainisha kuwa zoezi hilo litaanza kikanda ambapo watakagua magari yanayosafirisha mafuta na vituo vinavyouza mafuta ili kuwadhibiti wafanyabiashara hao ambao wamekuwa wakichanganya mafuta kwenye vituo hivyo.
Bwana KAGUO amesema magari yatakayokutwa yamechanganya mafuta kwa mujibu wa kanuni ya Bunge iliyotungwa mwaka 2010, dereva wa gari hilo atatozwa Shilingi Bilioni mbili kama faini ya kufanya uharibifu huo.
.

No comments: