Tuesday, August 30, 2011

Answar Sunnah wameshakula Idd yao!!

Na Benect Komba-Pwani.

Waislamu wa madhehebu ya ANSWAR SUNNAH mjini Kibaha mkoani Pwani leo
hii wamesheherekea sikukuu ya kuzaliwa Mtume MUHAMMAD SAW, kwa kuaswa
kuendeleza kutenda mema kama vile walivyofanya walipokuwa katika
mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Imam wa msikiti wa AL- FURKAN wa mjini Kibaha, HALIFA ISMAIL KWEKA
amesema kufunga ni sawa na muumini kuwa chuoni na anapotimu masomo
hategemewi kuwa kama alivyokuwa awali, hivyo amewataka waislamu
kuhakikisha wanaendeleza mema yote ambayo walikuwa wanafanya katika
kipindi chote cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

IMAM KWEKA amewaasa waislam nchini kusheherekea sikukuu hiyo kwa
kufanya mambo kwa kadiri bila kumchukiza muumba, kwa kufanya mambo
yasiyofaa ambayo ni machukizo kwa mwenyenzi Mungu, kwa upande mwingine
IMAM KWEKA amehimiza mshikamano, upendo na huruma miongoni mwa
Waislamu ili waweze kusaidiana panapokuwapo matatizo.

Aidha amehimiza kuboreshwa kwa vituo vinavyotoa elimu ya kiislam, ili
kutoa fursa kwa vijana wa kiislam kuielewa misingi na taratibu za
kiislam ili kuwa na jamii yenye kumuogopa na kumheshimu Mungu katika
kipindi watakachokuwepo duniani.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa kituo kinachotoa mafunzo ya dini ya
Kiislam cha DARUL ARQAM LEARNING CENTRE, MUDIR MUHAMMED TUNDIA
ameelezea kuhusu tofauti ya siku ya kufungua kati ya wao na wenzao,
ambapo amefafanua kimsingi Mungu utoa baraka zake katika sala yoyote
inayoswaliwa na waislamu wote kwa pamoja lakini kutokana na sababu
ambazo hazipo wazi kumekuwa kuzuka mgogoro kila inapofika siku ya
mwisho ya mfungo wa Ramadhan.

Amesema wao kwa upande wao wamesheherekea sikukuu ya IDD EL FITR
kufuatia taarifa ya kuonekana kwa mwezi Mkoani Lindi na taarifa
kuhusiana na kuandama kwa mwezi kupelekwa baraza kuu la waislamu
Tanzania -BAKWATA- kwa ajili ya kutangazia umma kitu ambacho
hakijafanyika, Kwa hiyo kwa upande wamenasheherekea sikukuu hiyo bila
kuwepo na tatizo na hasa ikizingatiwa suala lenyewe ni la kiimaniu.

No comments: