Thursday, September 22, 2011

HABARI NJEMA KWA VYUO VYA ELIMU YA JUU NCHINI

Lacture room UDSM
Tanzania itafaidika na msaada wa Euro Milioni 15 sawa na zaidi ya Bilioni 30, toka serikali ya Uholanzi kugharamia mradi wa Kujenga Uwezo kwa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini, unaojulikana kwa jina la NICHE

Meneja wa mradi huo, Bi.UTE JANSEN, amesema hayo alipotembelea Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo ambao kwa chuo kikuu hicho utafadhili Shule ya Biashara na kuboresha mafunzo ya utawala wa Serikali za Mitaa.

Bibi, JANSEN, amesema ana matumaini makubwa sana kuwa mradi huo utakapokamilika, utaboresha sekta zilizoainishwa kwenye mradi huo ambazo ni kujenga uwezo katika kutoa elimu kuhusu Afya, Sekta Binafsi na Serikali za Mitaa.

Msimamizi wa mradi huo hapa nchini kupitia Shirika la NUFFIC, Bibi JOHANNA VAN NIEUWENHUIZEN, amesema Uholanzi imeridishwa sana na jinsi Tanzania inavyoitumia misaada toka nchini mwake, hivyo kujihakikishia fursa zaidi za kusaidiwa katika miradi mbalimbali.

Naye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa  MUGISHI NKWABI MGASAameishukuru serikali ya Uholanzi kwa kufadhili mradi huo na kueleza kuwa ufadhili huo unamaana kubwa sana kwa Chuo Kikuu cha Mzumbe, kwa sababu utapanua uwezo wa chuo hicho katika kutoa mafunzo ya biashara na utawala wa serikali za mitaa.

No comments: