Thursday, September 22, 2011

BP WASALIMU AMRI, WAOMBA RADHI WATANZANIA

Kampuni ya Mafuta ya BP imeiomba radhi serikali, wateja wake na wananchi kwa usumbufu walioupata wakati walipofanya mgomo hali iliyosababisha Mamlaka ya Udhibiti wa Mafuta na Maji (EWURA), kuifungia leseni ya uagizaji mafuta ya kampuni hiyo.

Kampuni hiyo imechukua hatua ya kufuta kesi ambayo iliifungua dhidi ya EWURA kwenye Mahakama ya Ushindani pamoja na kuirudishia EWURA gharama ilizotumia kujitetea kwenye kesi hiyo.


 Mkurugenzi wa EWURA Bwana HARUNA MASEBU ameeleza kuwa baada ya BP kuomba radhi, EWURA imeona hakuna sababu ya kuendelea kuifungia kampuni hiyo kwa muda mrefu zaidi.

No comments: