Saturday, June 25, 2011

Onyo kwa Madereva wa Boda Boda

Mkuu wa wilaya ya MOSHI ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi
na usalama ya wilaya hiyo Alhaji MUSSA SAMIZI amemuagiza kamanda wa
Polisi wa wilaya ya MOSHI kuwachukulia hatua kali waendesha pikipiki
wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu.

SAMIZI amesema baadhi ya waendesha pikipiki wanaobeba abiria wamekuwa
wakijihusisha na wizi wa mali za abiria jambo ambalo linahatarisha
usalama wa abiria hao.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake SAMIZI amesema kamati
ya ulinzi na usalama imekuwa ikipokea taarifa kwa wananchi mbalimbali
juu ya vitendo vya kuibiwa mali zao na waendesha pikipiki hasa nyakati
za usiku.

Hata hivyo baaddhi ya wakazi wa eneo ya SOWETO wamesema vitendo vya
kuibiwa na waendesha pikipiki vimekithiri sana na hivyo hatua ya
kamati ya ulinzi na usalama kuingilia kati suala kutasaidia kupunguza
vitendo hivyo.

No comments: