Thursday, August 18, 2011

Hii imekaaje hii!!


Kiongozi wa kanisa Katoliki pop Benedict wa 16 anakwenda Madrid leo kuhudhuria tamasha la siku nne la vijana ambalo limetanguliwa na maandamano ya kumpinga kiongozi huyo wa dini. Jana Jumatano watu 5,000 waliandamana katikati ya mji wa Madrid wakipinga gharama zilizotumika za euro milioni 50 kwa ajili ya tamasha hilo huku kukiwa na hali ngumu ya uchumi pamoja na masuala mengine kadha, ikiwa ni pamoja na upinzani wa kanisa katika haki za mashoga pamoja na msimamo wa wazi wa kuliondoa kanisa katika masuala ya serikali. Polisi imesema kuwa watu sita wamekamatwa na maafisa wawili wa polisi wamejeruhiwa. Watayarishaji wa tamasha hilo la vijana wa Kikatoliki wamesema kuwa gharama za tamasha hilo zinagharamiwa kutokana na malipo ya ushiriki pamoja na michango. Zaidi ya watu milioni moja wanatarajiwa kukusanyika mjini Madrid. Kiongozi huyo wa kidini anatarajiwa kuongoza sala maalum ya usiku pamoja na misa ya wazi mwishoni mwa juma.

No comments: