Sunday, February 6, 2011

Ibada!

Wakristo nchini wametakiwa kutambua kuwa kanisani siyo mahali pa kukusanya fedha bali ni mahali pa maombi na kupata baraka kwa njia ya kumtolea Mungu sadaka kwa ukamilifu wa moyo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dakta ALEX GEHAZ MALASUSA wakati akihubiri kuhusu kumtolea Mungu kwa moyo wa ukamilifu katika ibada ya siku ya Bwana katika kanisa kuu la Azania Front leo jijini Dar es Salaam.

Askofu Dakta MALASUSA amewataka wakristo wafahamu kuwa sadaka si mali ya kanisa bali ni mali ya Mungu na kwamba ipo faida kubwa katika kutoa sadaka kwa ukamilifu.


Amesema kuwa maandiko matakatifu yanafundisha kuwa Mungu haangalii ukubwa wa sadaka bali anaangalia moyo wa mtoaji hivyo wakrito wasitoe kama utamaduni bali watoe kwa moyo ili kuruhusu neema ya Mungu ifanye kazi ndani ya maisha yao na watambue sadaka si jambo la kawaida kwa kuwa inagusa moyo wa Mungu.

Ibada hiyo ya siku ya Bwana ya tano baada ya ufunuo imeongozwa na baba Askofu Dakta ALEX GEHAZ MALASUSA na Msaidizi wa Askofu GEOGRE FUPE, Chaplain wa Kanisa Kuu, Mchungaji CHEDIEL LWIZA na Mkuu wa Jimbo la Kati Mchungaji ASTON KIBONA.

No comments: