Saturday, February 12, 2011

TAARIFA-UCHAGUZI TZ!!

Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi Mkuu Nchini Tanzania, Bwana DAVID MARTIN, amewasilisha taarifa ya mwisho leo kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka jana.

Ujumbe wa Waa

ngalizi wa Uchaguzi wa Juimuiya ya Ulaya (EU EOM) ulikuwepo nchini kuanzia Septemba 29 hadi Novemba 28, mwaka jana, kufuatia mwaliko wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya hapa nchini.

Ujumbe wa EU EOM ulisambaza waangalizi wa uchaguzi 103 katika mikoa yote 26 nchini kutoka nchi zote 27 wanachama wa Jumuiya ya Ulaya pamoja na nchi za Canada, Norway na Switzerland ili kufuatilia kwa umakini jinsi gani mchakato mzima wa uchaguzi ulikuwa ukiendeshwa kulingana na kanuni na mapatano ya kimataifa na kikanda pamoja na sheria za Tanzania.

Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi Bwana DAVID MARTIN, Mbunge katika Bunge la Ulaya amesema lengo la taarifa hiyo ya mwisho ni kutoa mapendekezo na ushauri wenye nia ya kudumisha demokrasia nchini Tanzania.

Ameeleza kuwa mapendekezo na ushauri vinavyotolewa katika taarifa hiyo haviilazimishi wala kuiamuru asasi au taasisi yoyote kuyatendea kazi bali yanapaswa kujadiliwa kwa kuzingatia historia, jiografia na mila na desturi za nchi hii.

Kutokana na majadiliano yaliyofanyika Bwana MARTIN amesema ana imani kuwa serikali, vyama mbalimbali vya upinzani, asasi za kiraia na umma watashiriki kikamilifu katika kujadili sheria na taratibu za uchaguzi zinazotakiwa kufanyiwa marekebisho.

Ripoti inatoa matokeo ya ufuatiliaji wa uchaguzi na mapendekezo ya kina yenye lengo la kuboresha chaguzi zijazo katika maeneo yote ya mchakato wa uchaguzi.

No comments: