Friday, February 4, 2011

Soma hii ya marehemu Shoga wa Uganda


Polisi nchini Uganda hapo jana imesema mwanaharakati mashuhuri wa kuteteta haki za mashoga aliyepatikana amefariki wiki iliyopita, aliuwawa na mpenzi wake. Hii inaondoa wasiwasi kuwa mauwaji hayo yalihusika na harakati zake za kutetea mashoga.

David Kato alipigwa kwa nyundo nyumbani mwake wiki iliyopita, na alifariki alipokuwa akipelekwa hospitalini.Tukio hilo limeshutumiwa vikali ulimwenguni na kuangazia masuala ya haki za mashoga nchini Uganda na mataifa mengine ya Afrika ambapo ushoga umepigwa marufuku.

Polisi imesema imemkamata Enock Nsubuga, ambaye walimtambulisha kuwa mwizi mashuhuri, nyumbani mwa mpenzi wake wa kike, na imesema amekuwa akiishi kwa Kato baada ya mwanaharakati huyo kumtoa kwa dhamana gerezani tarehe 24 mwezi wa Januari. Afisa mkuu wa polisi Uganda, Inspekta jenerali Kale Kayihura, jana aliwaambia waandishi habari kuwa kwa mujibu wa mshukiwa huyo, alijaribu kujadiliana na marehemu kumlipa pesa kwani walikuwa na uhusiano wa kimapenzi. Kayihura alisema kuwa wawili hao walishiriki ngono, lakini Kato hakuilipia huduma hiyo.

No comments: