Friday, February 4, 2011

Breaking Newz-Mubarak yu tayari kuondoka!!!




Makamu wa Rais wa Misri, amewahakikishia wamisri kuwa Rais Hosn Mubarak ambaye waandamanaji nchini humo wanatimua kivumbi kumtaka ajiuzulu, atajiuzulu hivi karibuni, lakini ana hofia kuiacha nchi hiyo katika mtibwiriko.

Leo Ijumaa, waandamaji wameiita siku hii kuwa ni ya kuondoka kwa Mubarak, huku kivumbi cha kumtaka ajiuzulu kikitimka katika miji mbalimbali nchini humo, huku wasanii, waigizaji, na watu mbalimbali maarufu nchini humo wakiungana na wananchi kumtaka rais huyo ajiuzulu.

Vikosi vya jeshi vimetanda nje ya uwanja wa Liberation Square, ambako takribani watu Milioni mbili wamekusanyika huku wakiimba nyimbo za kumtaka Mubarak aachie ngazi.

Ripoti makini inafuatilia kwa makini sakata hili, na tangu lianze, leo ni siku ambayo angalau, Mubarak ametangaza kwamba yuko tayari kuachia ngazi.

No comments: