Thursday, July 21, 2011

Pinda akemea wapinzani

Waziri Mkuu MIZENGO PINDA ameelezea kusikitishwa kwake na taarifa za kuwepo baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini wanaobeza muafaka wa kisiasa uliofikiwa visiwani Zanzibar na kusababishwa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani humo.

Waziri Mkuu PINDA ametoa rai hiyo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu baada ya mbunge wa Wawi HAMAD RASHID MOHAMED kudai kuwepo kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaotumia vyombo vya habari kubeza muafaka huo ambapo Waziri Mkuu amehadharisha uhakika wa habari wa baadhi ya magazeti.

Mheshimiwa PINDA amesema kama ni kweli wapo watanzania wanaoweza kukejeli hatua nzuri iliyofikiwa visiwani Zanzibar ya kujenga umoja wa kitaifa ndani ya serikali ya visiwa hivyo basi watanzania hao wana upngufu.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu PINDA ameeleza kuwa serikali haijashindwa kutafuta suluhisho la tatizo la magao wa umeme unaoendelea hapa nchini na kusema kuwa hivi sasa serikali inafanya jitihada za kutafuta Megawati za ziada katika kupunguza makali ya mgao huo.

Kuhusu kutokutoa maamuzi kuhusu suala la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini aliyeandika barua akizitaka taasisi zilizo chini ya wizara yake kutoa kiasi cha Shilingi Milioni 50 ili kuwezesha kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo, Waziri Mkuu amesema kuna kikomo cha mamlaka katika maamuzi kwa yule aliyeachiwa madaraka endapo Rais hayupo hapa nchini.

No comments: