Friday, August 19, 2011

Kawambwa atoa ufafanuzi!!


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dokta SHUKURU KAWAMBWA ametoa taarifa ya tume ya Rais iliyopewa kazi ya kuchunguza na kushauri namna nzuri ya utoaji wa mikopo ya elimu ya Juu hapa nchini ambapo mabadiliko makubwa yamejitokeza ikiwemo fedha kuanza kutolewa na Vyuo husika badala ya Bodi ya mkopo ili kumaliza tatizo la kulipa wanafunzi wasio vyuoni.

Waziri KAWAMBWA ametoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari Mjini DODOMA na kuongeza kuwa Bodi ya mikopo itaratibu utoaji wa ruzuku kwa wanafunzi wa sayansi za tiba kuanzia mwaka huu wa masomo.

Katika hatua nyingine Waziri KAWAMBWA amesema Tume hiyo iliyoundwa na Rais JAKAYA KIKWETE mwezi wa pili mwaka huu imebadili utaratibu wa urejeshaji mikopo badala ya kurejesha kwa miaka kumi tu hivi sasa mhusika atakatwa asilimia nane ya mshahara wake mpaka atakapomaliza deni lake ili kutowaumiza walipaji kutokana na kipato kidogo wanachopata.

Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wamekuwa wakilalamikia kutopata mikopo yao kwa wakati hali iliyomfanya Rais KIKWETE kuunda Tume ili kutatua tatizo hilo.

No comments: