Thursday, February 3, 2011

KARIBUNI WADAU

Wadau wote wa blogs,
Nawakaribisha sana katika blog hii, ambayo ni mahususi kwa ajili ya kuripoti habari mbalimbali kwa kuzingatia kile ambacho wewe mdau unakitaka, kuhusiana na masuala mbalimbali yanayotuhusu katika jamii yetu.

Labda niseme tu kwamba, tasnia ya blog, inakua kwa kasi hata kwenye nchi maskini kama Tanzania.
Kwa kutambua fursa hii, na kwa kuzingatia kwamba mimi ni mwana mawasiliano na ni mwanahabari ninayefanya kazi Uandishi wa habari na Utangazaji kwa miaka kadhaa sasa, nina kila sababu ya kukupa habari wewe mdau.

Aidha, changamoto kubwa zinazoikabili jamii ya sasa, hususan utandawazi na sakata la kumomonyoka kwa maadili miongoni mwa jamii hasa vijana, vinachangiza umuhimu wa kuwa na chombo kama hiki, kwa lengo la kurudishana katika mstari iwapo kuna mtu anafanya ndivyo sivyo.

kwa ujumla, nawakaribisheni sana, mshiriki pamoja nami katika ndoto hii ya siku nyingi ambayo leo, inatimia kiukwelikweli,
Ahsanteni na Karibuni sana kwa mara nyingine.
Isaac SIfa Kikula,
Dar es Salaam-Tanzania

No comments: