Thursday, August 25, 2011

Vinara wizi wa pikipiki mbaroni.


Jeshi la polisi mkoa PWANI limewatia mbaroni watu wawili kwa tuhuma za kumteka na kumua dereva wa pikipiki aina ya bajaji bwana SEIF OMARI MAPUNDA mkazi wa mbagala jijini DSM na kisha kuiba pikipiki hiyo.

Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa PWANI SSP EVANCE MWIJAGE amesema maiti ya dereva huyo imeokotwa kikiwa imetupwa kandokando ya barabara ya Morogoro ikiwa na jeraha kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na pia ukiwa umechomwa sehemu za tumboni.

Kamanda wa polisi mkoa wa PWANI ERNEST MANGU amesema baada ya msako polisi iliwanasa watuhumiwa wakiwa na matairi ya bajaji hiyo pamoja na speed meter mbili breek na spana na baada ya kuojiwa kwa kina walionyesha pikipiki hiyo yenye namba za usajili T 657 BTJ ikiwa imefichwa kwenye shamba la mpunga.

Amewataja watuhumiwa kuwa ni MAULID RAJABU na HASSANI HARUNA wote wakazi wa KIBAHA mkoani PWANI.

Watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho.

No comments: